Header

SAFARI YA BEKA THE BOY KIMUZIKI YAZIDI KUTIA FORA!

 

Msanii kutoka nchini Kenya Beka the Boy kwasasa hashikiki kimuziki. Japo alianza kwa mwendo wa kuchechemea ila kwasasa muziki wake umeshika kasi. Ukumbuke Beka the Boy nikati ya wasanii wale wachache wa Afrika mashariki wanaokuwa na uwezo wa kumiliki recording label zao wenyewe. Yeye ndie raisi wa lebo ama nembo ya muziki nchini Kenya kwajina DoubleB, ambayo pia inasimamia kazi zake zote za muziki na kibiashara. Kwa hivi sasa msanii huyu, ameonekana kutokea kupendwa na kuwa na mashabiki lukuki haswa kutoka jiji kuu la Kenya Nairobi kwa hulka ya kuitumia lugha ya Kiswahili sanifu kitu kinacho wachanganya wengi wakidhania anatokea hapa Tanzania.

Nembo ya DoubleB

Imebainiaka kuwa Beka the Boy, amekuwa akiongoza wasanii wenzake katika hali ya kutangaza sera zake za muziki. Huku akiwa kwasasa ndiye msanii pekee anayefikia media nyingi zaidi nchini Kenya siku baada ya nyingine. Akiongea na meza yetu ya habari ya Dizzim, Beka the Boy anasema yakuwa, sababu kuu ya kufanya hivyo nikuhakikisha kuwa muziki wake unawafikia watu wengi zaidi haswa ndani na nje ya nchi ya Kenya. Beka the Boy ameoneka kuwa ananjaa ya kuipiku na kuiongoza sanaa ya muziki wa Kenya huku wiki jana pekee akiwa kazifikia media zaidi ya nne ikiwemo Kiss 100, East Africa Magic, Bahari fm na zinginezo.

Beka the Boy wapili kutoka kushoto akiwa na wadau wa muziki wa kituo cha redio cha Hot 96

Katika swala la kutoa muziki wa viwango vya kimataifa pamoja na video, Beka the Boy amelivalia njuga swala hili huku akinadi kuwa bila ya kufanya hivyo basi ingemuia ugumu kufikia malengo ambayo ameyafikia kwasasa. Beka the Boy kwasasa anatamba na kibao chake kipya kwa jina Level ambacho kimezidi kushika chati mbalimbali za muziki ikiwemo BoomPlay pia. Bidii yake ya mchwa inafanya aangaziwe zaidi na vyombo vya habari Kenya nakupata mialiko mingi ya interview siku baada ya nyingine.

Beka the Boy akiwa kwenye interview ndani ya Kiss 100

 

Beka the Boy akiwa na mtangazaji Tuva wa radio Citizen

Comments

comments

You may also like ...