Header

Mbwana Samatta alaani kitendo cha kupigwa kwa Mwandishi wa Habari ‘Sillas Mbise’

Nyota wa mpira wa miguu kutoka Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk, Mbwana Ally Samatta amelaani kitendo cha kushambuliwa kwa Mwandishi wa Habari za Michezo, Sillas Mbise.

Tarehe 8 Agosti mwaka huu, Mwandishi Mbise alishambuliwa na Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba SC ya Tanzania na Asante Kotoko ya kutoka nchini Ghana.

Mbwana Samatta aliandika kwenye Ukurasa wake rasmi wa Twitter. “Sio kitendo cha kiungwana askari kupiga mwandishi katika eneo la michezo,mpira ni mchezo unaoleta amani sio kuvunja amani.”.

Comments

comments

You may also like ...