Header

Familia ya Bobi Wine yajawa na Hofu baada ya kifo cha Dereva wake

Mwanamuziki maarufu nchini Uganda na mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki, Bobi Wine amenusurika kifo baada ya gari lake kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Arua kaskazini magharibi mwa Uganda.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu hii ambapo Bobi Wine alithibitisha kifo cha Dereva wake anayefahamika kwa jina la Yasiin Kawuma ambaye alishambuliwa vibaya kwa risasi hadi umauti.

Hata hivyo Mke wa Bobi Wine, Bi. Barbie Kyagulanyi aliutumia ukurasa wake wa Facebook kuzungumzia hali hiyo ya tukio na kudai kuwa mpaka sasa Mmewe na wenzake saba haijulikani wako wapi na wako kwenye hali gani.

Friends and Family; it's a dark night tonight. As you all know;our driver has been shot dead in Arua. It's a very sad…

Posted by Barbie Kyagulanyi on Monday, August 13, 2018

Comments

comments

You may also like ...