Header

Lord Eyez Atokeza kichwa chake Weusi akiwa na Joh Makini na S2Kizzy

Staa wa muziki wa Rap kutoka Tanzania, Lord Eyez ameanza kuonekana akiwa katika muonekano mpya na inahisiwa kuwa kuna ushirikiano wa kilichofanyika kati yake na Rapa Joh Makini katika Studio za Switch Records.

Rapa Eyez mbali na kuwa ameonekana kwenye video ya wimbo mpya wa Joh Mkaini ‘Simwachii Mungu’ ft. Ben Pol, siku kadhaa zilizopita aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa Studio na Joh Makini pamoja na Producer S2kizzy ambapo alidai kuwa kuna kilichofanyika kati yao.

Issa session#godsons#iende@johmakinitz@bontamaarifa@s2kizzy

A post shared by LORDEYES (@lordeyesmweusi) on

Aidha inahisiwa kuwa, Lord Eyez anaweza kuwa amerudisha mahusiano ya karibu yenye misingi imara na Weusi Kampuni kama zamani. Kwa muda usiopungua miaka mwili mpaka sasa Lord Eyez alibaki katika sintofahamu bila kauli iliyonyooka juu ya uwepo wake rasmi katika umoja wa Kampuni hiyo.

Hata hivyo msemaji na mwanafamilia wa Kampuni hiyo, Nikki wa Pili bado hajatoa kauli wala tamko la uwepo wa Lord Eyez kwenye umoja wao unaoundwa na Joh Makini, G Nako na Bonta Maarifa. Weusi wanafanya vizuri na wimbo wao kwa jina ‘Mdundiko’ ambao Lord Eyez hakushiriki.

Comments

comments

You may also like ...