Header

Bobi Wine ashindwa kutembea akiwa mikononi mwa Polisi

Msanii wa muziki na Mbunge nchini Uganda, @bobiwine amejeruhiwa vibaya kiasi cha kushindwa kuongea na kutembea mwenyewe.

Bobi anadaiwa kupigwa vibaya na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchini humo, hali hiyo ilithibitishwa na mwanasheria wa msanii huyo, Bw. Asuman Basalirwa.

Bobi Wine aliingia kwenye mikono ya Sheria ambapo ameshtakiwa Mahakamani kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria.

Mtu mmoja kwa jina la Yasiin Kawuma ambaye alikuwa ni Dereva wa msanii huyo aliuwawa kwa risasi jumatau ya wiki hii akiwa kwenye gari katika tukio linalosemekana kuwa lilikuwa ni jaribio la kumuua Bobi Wine.

Bobi Wine alikamatwa baada ya gari lililokuwa kwenye msafara wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni kushambuliwa siku ya Jumatatu katika mji wa Arua nchi humo.

Comments

comments

You may also like ...