Header

Lizer Classic ndani ya Wasafi Records, ashirikiana na Mmarekani kupitia Mandi Classic

Msani wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kongo, Mandi Classic amezungumzia kufanikisha kolabo iliyowakutanisha Mtayarishaji kutoka Marekani na Mtayarishaji Lizer kutoka Tanzania kwenye kazi yake mpya ‘FRESHMA’ aliyomshirikisha, Martin Classic.

Mandi Classic

Akipiga Stori na Dizzim Online, Mandi amesema kuwa Mtayarishaji Big Zo kutoka nchini Marekani aliwarekodi sauti za kazi yao hiyo, kisha zikatumwa kwa Lizer ambapo baadae utayarishaji ulikamilika chini ya Lizer nchini Tanzania katika Studio za Wasafi Records.

Big Zo

“Producer aliyetutengenezea Sauti hapa U.S.A na kuzituma kwa Lizer anaitwa Big Zoo, ni Marekani Mweusi ambaye ni mwanamuziki pia. Alipenda sana kusikika Mixing ya Bwana Lizer na haijui sana Tanzania na kazi yangu hii ni kazi yake ya kwanza kufanya na mtu wa nje ya Marekani” Alisema Mandi Classic.

Aidha Mandi aliongeza kuwa, Kushirikiana kwake na Martin na kufanana kwa matumizi ya ‘Classic’ mwisho wa majina yao haina maana kuwa wawili hao ni kundi bali ilitokea kila mmoja akawa anajiita hivyo kitu ambacho walipokea maswali ya wengi kutaka kujua kama wao ni muunganiko wa kundi.

Video ya wimbo ‘FRESHMA’.

Comments

comments

You may also like ...