Header

Madee, Dogo Janja kuipamba Bundesliga Msimu 2018/2019

Kwa sasa Makampuni mbalimbali nchin yameona tija sana kuwapa Dili nono Mastaa wa Bongo kuhakikisha wanafikisha Ujumbe au kutangaza Bidhaa zao. Hii Leo Mastaa wawili wa Muziki wa Bongo Fleva Madee Ali pamoja na Dogo Janja wametambulishwa Mbele ya Waandisi wa Habari kuwa Mabalozi wa Kampeni hii ya  Ligi ya Bundesliga kwa kiswahili, Mastaa hao watafanya nao kazi katika kuhakikisha taarifa zinafika kwa wakati wateja ambao muda mwingi wanakuwa katika mitandao ya kijamii.

Ligi ya Ujerumani ni miongoni mwa ligi kubwa na bora kabisa barani ulaya, ikiwa na wachezaji mahiri kama mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Lewandowski, Marco Reus, mjamaica Leon Bailey na wengine wengi. Katika msimu huu wa 2018/19  Kampuni ya StarTimes imeisogeza Burudani zaidi ya Bundesliga kwani itakuwa ikitangazwa Michezo yote hiyo kwa lugha ya Kiswahili. Mbali na ligi ya Bundesliga, StarTimes pia ni warushaji wa ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ambayo ina mastaa kama Neymar na kinda machachari Kylian Mbappe. Ligue 1 ambayo imeanza takribani wiki mbili zilizopita inasifika sana kwa kuwa chimbuko la vipaji vingi ambavyo vinatamba katika ligi mbalimbali. kwa sasa Kampuni hiyo ya StarTimes ndio kampuni pekee ambayo ina haki ya kurusha Matangazo ya Ligi hiyo moja kwa moja kupitia King’amuzi chao cha StarTimes kwa Watumiaji wa Dishi pamoja na Antena.

Comments

comments

You may also like ...