Header

PRODUCER EMMY DEE KUAMSHA ARI YA MUZIKI WA MOMBASA TENA!

Producer Emmy Dee

 

Nikati ya watayarishi wa muziki wakongwe zaidi kuwahi kutokea hapa Africa Mashariki. Heshima yake katika ulimwengu wa muziki niwahaiba yake, katika miaka ya nyuma alishawihi kuwahifadhi wasanii tajika wa hapa Tanzania kila walipoingia mji wa Mombasa kwa shughuli zao za kibiashara ikiwemo kutoa burudani kwa mashabiki wao wa nchini Kenya, akiwemo Mr. Blue na wengineo. Mtayarishi huyu wa muziki wakizazi kipya mwenye makazi yake mjini Mombasa na mmiliki wa studio maarufu na kongwe zaidi nchini Kenya kwa jina Jungle Masterz, amehusiki zaidi kuwatoa kimuziki wasanii wakubwa wa muziki tokea Kenya, wakiwemo mastaa kama Sudi Boy na Dogo Richie a.k.a Rich Ree miongoni mwa wengine wengi ambao nikianza kuwataja huenda ukurasa huu usitoshe.

Nembo ya studio ya kutayarishia muziki ya Jungle masters

Emmy Dee anamikakati kabambe ambayo ameiwekea misingi ya kipekee kuhusiana na kuirudishia sanaa ya pwani hadhi yake ya juu kama ilivyokua zamani. Akiongea na meza yetu ya habari ya Dizzimonline, Emmy Dee aka mshale bora mwituni, amehakikishia mashabiki wake kwamba kwasasa yupo tayari kuanza kuachilia vibao vipya alivyokuwa akivishughulikia vinavyo jumuisha wasanii wake wa zamani ama mastaa walioibuka kupitia mikono yake na chipukizi wanaoibuka ilimradi kuirudishia Pwani ya Kenya utukufu wake kama ilivyokua nyakati zile za zama. Emmy aalinadi kuwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, alikuwa anaptia changamoto nyingi si haba zakutaka kuiboresha studio yake ili iwe na hadhi ya kisasa kitu ambacho kilimfanya kurudi nyuma kiasi lakini kwasasa ndoto yake ya kuiboresha studio ya jungle Masterz imekamilika nandiposa anahisi huu ndio wakati mwafaka wakuachilia vibao vipya chini ya studio mpya iliyoboreshwa kwa mitambo ya kidijitali na kisasa itakayoweza kuhimili ubora wa bidhaa za muziki mtamu zaidi na wakukubalika kimataifa.

Comments

comments

You may also like ...