Header

Baada ya Diamond Platnumz, Mtanzania mwingine afanikisha Kolabo na Mwimbaji kutoka Zimbabwe

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, K Single amefanikiwa kuuleta pamoja mchanganyiko wa wakali wa muziki kutoka Zimbabwe na Afrika Kusini kwenye kazi yake mpya na ya kwanza kwa jina ‘Wakanaka’ katika Studio za Deep Sound.

K Single

K Single mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita aliachia rasmi wimbo wake huo aliomshirikisha Mwimbaji Willionair Africa kutoka Zimbabwe. Wimbo huo uliotayarishwa kwa ushirikiano wa Producers wawili kutoka nchini Afrika Kusini, Deep Sound Crew na Mr Freshly chini ya Deep Sound Studio.

 

Willionair Africa

Video ya wimbo huo imeongozwa na Muongozaji Bwana Mtui kutoka Tanzania aliyeishi kwa miaka kadhaa mpaka sasa nchini Afrika Kusini.

Itakumbukwa kuwa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ni msanii wa kwanza kufanikisha kolabo iliyounganisha muziki wa Tanzania na Zimbabwe kupitia kolabo ya wimbo wa ‘Watora Mari’ alioshirkishwa na Jah Prayzah.

Itazame Video ya wimbo hapa nchini.

 

Comments

comments

You may also like ...