Header

Kriswill aingia mkataba mmoja na lebo iliyomsaini mwalimu wa Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Nigeria, Kriswill amedaka mkataba wa kufanya kazi za muziki chini ya usimamizi wa lebo ya Shine Records ya nchini Afrika Kusini.

Kriswill

Akizungumza na Chumba cha Habari cha Dizzim Online, Mkurugenzi wa lebo hiyo ya muziki, David Kennedy Shine amesema kuwa kwa sasa mbali na kufanya kazi na wasanii wasiopungua saba chini ya lebo hiyo, Kriswill ameingia kwenye usimamizi mmoja wa kazi na aliyewahi kuwa Mwalimu wa lugha ya Kiingereza wa msanii Diamond Platnumz anayefanya muziki kwa sasa, Teacher Allen.

“Nilipenda kipaji chake ndo maana nilimsani, Mkataba wake umeanza rasmi tarehe 15 mwenzi huu na unaweza kuona tayari tumeachia kazi yake ya kwanza. Mbali na kuwa anajua anachokifanya, sioni sababu ya kumsubirisha kwakuwa ana viwango ya kwenda kimataifa mapema kabisa kwa nianchokiona ndani ya uwezo wake” Alisema David Kennedy Shine.

Kriswill baada ya kauchia audio ya wimbo wake wa kwanza chini ya lebo hiyo unaokwenda kwa jina ‘Sumthin’, kwa sasa yuko katika hatua za mwisho ili aweze kuachia rasmi video ya wimbo wake huo muda wowote kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.

Wasanii wengine wanaofanya kazi nchini ya lebo hiyo ni pamoja na Teacher Allen, Mr Paul, Kmilex, Lilianinternet, Nanal Cool, Niva na Solution. Teacher Allen kwa sasa anafanya vizuri na wimbo unaokwenda kwa jina ‘Chakubimbi’.

Sikiliza wimbo wake unaokwenda kwa jina ‘SumThin’ hapa chini.;

Comments

comments

You may also like ...