Header

Major Lazer waachia nyingine wakiwa na staa wa SA, Babes Wodumo

Major Lazer wameachia wimbo mpya, Orkant/Balance Pon It wakimshirikisha muimbaji wa Afrika Kusini, Babes Wodumo. Wimbo huo umekuja na video mpya ya ushirikiano kati Major Lazer na muongozaji wa Afrika Kusini, Adriaan Louw. Video hii imefanyika huko jijini Durban.

“Orkant/Balance Pon It” imekuja baada ya kuachiwa kwa “All My Life” ikimshirikisha nyota wa Nigeria, Burna Boy na ni wimbo wa pili wa wa ushirikiano na wasanii wa Afrika kutoka kwa Major Lazer.

Major Lazer hivi karibuni pia walizindua Afrobeats Mix mpya, yenye mchanganyiko wa nyimbo toka barani na kutumia jukwaa lao la kimataifa kuonesha uwezo wa wasanii wa Afrika.

Pia, bendi hiyo itaanza ziara yake ya Afrika kuanzia mwezi huu hadi October kwa kupita nchini Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Ethiopia na Uganda.

Comments

comments

You may also like ...