Header

Babu Tale Amvisha taji la uhodari Zari The Bosslady

Meneja wa muziki wa msanii Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale a.k.a Babu Tale, amemvisha taji la uhodari mfanya biashara kutoka Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Zari the Bosslady kwenye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Zari ambaye anatimiza umri wa miaka 38, Babu Tale alimtaja kuwa ni mwanamke mwenye heshima na hodari aliyeiwakilisha vyema nchi yake, Sifa iliyogongana na baadhi ya mawazo watu kuwa alimtaja kwa namna yake ya kuwa ni mwanamke aliyempatia heshima ya watoto wawili msanii Diamond Platnumz, Tiffah na Nilan.

Zari ni mwanamke kati ya wanawake wachache wanaopewa heshima kutokana na misimamo katika baadhi ya maamuzi na aina ya maisha nayaoishi ndani na nje ya mitandao ya kijamii akilinganishwa na wanawake wengine waliowahi kutajwa kuwa wapenzi hata wa msanii Diamond Platnumz.

Comments

comments

You may also like ...