Header

Brown Mauzo aivutia Picha ndoa ya Wema Sepetu

Staa wa muziki kutoka nchini Kenya na hitmaker wa wimbo ‘Zagada’ Brown Mauzo ameshangazwa na hali ya kuchelewa kwa ndoa ya Mrembo Muigizaji na Staa wa filamu kutoka Tanzania, Wema Sepetu.

Wema Sepetu

Akizungumza na Dizzim Online, Brown amesema kuwa moja ya vitu vitakavyolipua na kuzungumziwa zaidi kwenye tasnia ya Burudani Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kama sio Afrika ni tukio na taarifa za Mrembo Wema Sepetu kufunga ndoa rasmi na kudai kuwa anashindwa kujua nini kinapelea kuchelewa kwa tukio hilo.

“Naamini Mrembo Wema ameshafikia umri wa mwanamke mzuri kuolewa, Pia wanaume wanauona uzuri wake lakini nashindwa kujua ni nini inahappen mpaka saa hii ya Ndoa haifungiki jamani.” Alisema Brown Mauzo.

Hata hivyo ilishaonekana kuwa Brown Mauzo alilisafiri mpaka Tanzania kulifata penzi la Wema Sepetu ingawa baada ya kuulizwa kama ni kweli aliingia Tanzania kwa lengo hilo alikana na kuruka mita mia.

 

Itazame Video ya Brown Mauzo – Killing Me.

Comments

comments

You may also like ...