Header

Mtayarishaji Shirko Atimiza ndoto nchini Kenya baada ya Kufanikiwa Tanzania

Mtayarishaji wa hit single kadhaa za Staa wa Bongo Fleva, Aslay na wasanii wengine Tanzania , Producer Shirko amefungua na kuitambulisha rasmi studio yake nyingine iliyopo nchini Kenya kwa jina ‘SHIRKO MEDIA ENTERTAINMENT’.

Akizungumzia hatua hiyo, Shirko ameiambiza Dizzim Online kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi kumiliki Studio kubwa na kwa sasa najivunia kuwa Boss wa kazi zake chini ya Studio hii mpya na ile ya iliyofunguliwa kabla, Vibe Records inayopatikana nchini Tanzania.

“Studio yangu Mpya nimeamua kuifungua Mombasa kwa sababu nyingi sana, Kwanza it is my home town, Pili ni kwamba kuna vilio vya wasanii wengi na wapya vikinikumbusha how i hustled. Vilio vya watu wengi vilikuwa vinahusiana na kwanini nawasaidia watu wengine nisisaidie vijana nyumbani” Alisema Shirko.

Comments

comments

You may also like ...