Header

Shaggie Bee atamani kolabo na Rapa YoungKiller Msodoki baada ya kumalizana na Kristoff

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Shaggie Bee amelitamani kolabo la Rapa YoungKiller Msokodiki kwenye ujio wa kazi yake itakayofuata.

Shaggie anayefanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Wangu’ aliomshrikisha Rapa Christoff, alisema kuwa muziki wake unapendeza zaidi pale anapomshirikisha mchanaji mwenye uwezo, hivyo kama sio kazi itakayofuata ana mpango wa kushirikiana na Youngkiller katika siku za usoni.

Young Killer Msodoki

“Muziki wangu una utamu wake nikimshirikisha na anayejua kuandika na kurap vizuri kama anavyofanya Msodoki wa Tz. Kama itashindikana kwenye my next project Basi nitaona vile itakuwa in my future Project coz is one of my favorite” Alisema Shaggie Bee.

Hata hivyo, Shaggie aliongeza kuwa sio kwamba anatengeneza mazingira ya kufanya vizuri kwa kolabo tu bali alisema hivyo kutokana na matokeo na maoni anayoyapata kupitia wimbo wake wmpya sokoni wa ‘Wangu’ alioshirkiana na rapa Kristoff.

 

Itazame Video ya wimbo ‘Wangu’ wake Shaggie Bee aliomshirikisha Kristoff.

Comments

comments

You may also like ...