Header

PREZZO: MSISHANGAE NIKIINGIA SIASA MWAKA 2022!

Rapper Prezzo

Rapper kutoka nchini Kenya na mmoja kati ya malejendari kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya maarufu kama Prezzo, amefunguka na kumwaga yake ya moyoni kuhusu kujiunga na siasa ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 nchini Kenya. Akiongea kwenye kipindi cha Ymashariki kinacho peperushwa hewani na runinga ya Y254 TV iliyopo na makazi yake jijini Nairobi, gwiji huyu wa miondoko ya mziki wa kufoka alimwambia mtangazaji wa zamu anayeendesha kipindi hiki cha burudani kwa jina Ken Rel Bis kuwa, hakuna kitu kisichowezekana. Nikinukuu kwa mkutadha maneno yake ” Mimi sioni kunaubaya kuingia kwenye siasa, kila kitu kinawezekana. Kwa mfano, miaka michache nyuma ungeniuliza swali kuhusu mheshimiwa Jaguar nisingekujibu ama ningepotezea. Ila kwasasa tunaweza ongea na hata kufanya kazi pamoja. Kwahivyo hata siasa pia naona wakati ukifika, basi naweza kujitosa ulingoni mzimamzima.” aliongeza.

Kutoka kushto, rapper Prezzo, Mtangazaji wa Y254 TV Ken Rel Bis(Katikati) na msanii pia mtayarishi wa mziki Yellow.

Akiongelea kuhusu kuwa na mahusiano na mrembo pia msanii kutoka hapa Tanzania maarufu kama Amber Lulu, Jaguar alionekana kulikwepa waziwazi swala hili, huku akibashiri kuwa watu hupenda kumuekelea maneno kwenye kinywa chake. Kwani kila wanapomuona ameshikana na mrembo yeyote vile basi wengi hunadi mara moja kuwa anatoka kimapenzi naye. ”Mimi naamini kuwa na mapenzi ya kirafiki sana, hivyo ninapokuwa na mwanadada yeyote silazima niwe natoka naye kimapenzi. Mbona basi watu wasiniiongelee kuwa natoka na Beyonce?” alimalizia kwa swali. Katika mahijiano hayo, Prezzo kuhusu kurudiana na aliyekuwa mchumba wake wa zamani Nick almarufu kama Sheila Mwanyiga, nguli huyu wa muziki alibaini kuwa maisha ni mviringo, hawezi sema kama wanaweza kurudiana wala la, kwani Mungu pekee ndiye anayepanga. ” Siwezi sema sana kuhusiana na swala hili, kwani naweza ongea mengi nikamaliza halafu ikatokea tukajarudiana halafu nyinyi tena mkaanza kunibeza na kukejeli kwanini nilisema hutuwezi rudiana.

Kutoka kushoto ni mtangazaji wa Y254 TV Ken Rel Bis, Prezzo, Dj Lesqa na msanii Yellow.

Prezzo katika usiku huo pia alimtambulisha msanii mpya na producer kwa jina Yellow. Natayari wawili hawa wameshatoa kibao kikali kwa jina ”Ready To Drink” ambacho tayari kinafanya vyema kwenye chati mbalimbali za muziki nchini Kenya. Prezzo pia alidokeza kuwa kwasasa ana shughulika na kuwasaidia wasio jiweza haswa watu wanaoishi kwenye vijitongoji duni kama vile Kibera. Akieleza kwanini alichagua kitongoji duni cha Kibera (Kibra) na wala si vijitongiji duni vingine vilivyomo jijini Nairobi, Prezzo alisema nikwasababu nafsi yake imekuwa ikivutiwa na mwendo mbiu msingi wa namna watu wa kibra wanavyoishi. Hivyo kupitia mradi wake wa kuboresha nyumba za wakazi wanaoishi kwenye hii sehemu, anapata furaha na amani moyoni mwake maana kila alalapo hujikumbusha kuwa kuna mtu mahali anafurahi pia kwakua anaishi kwenye nyumba iliyobora kuliko awali kupitia mikono yake. Hebu jionee mahojiano yote kupitia video hii iliyopo kwenye Youtube ya Ymashariki kwa mengi zaidi.

Comments

comments

You may also like ...