Header

MFAHAMU BEN C MSANII WA MUZIKI WA NJILI KUTOKA KENYA!

Nchini Kenya haswa jijini Nairobi muziki wa njili maarufu kwa wakenya kama (Gospel music) huwa ndio unopewa kipao mbele kwa sana. Japo muziki wa kidunia ama (Secular) pia unashika ila utakuta gospel unanafasi zaidi. Utakubaliana na mimi kwa njia ya mifano, ikiwa wasanii walioanza kupiga muziki wa kidunia wanao tokea jijini Nairobi kwa asilimia kubwa wamegeuka na kuingilia kufanya muziki wa gospel. Tukianza na Size 8, Wahu na Amani miongoni mwa wasanii wengine wengi tu waliojipatia majina kupitia muziki wa secular awali wote kwasasa wanaimba gospel.

Msanii Ben C (Kulia) akiwa na msanii/mtangazaji wa kipindi cha gospel cha kubamba kinachorushwa na Citizen Tv nchini Kenya.

Ila kwasasa sijataka kuleta mdahalo wa kiburudani, ila kukutambulisha kwa msanii anayetamba kupitia kibao chake kipya cha gospel kwa jina Roroa, ambacho kina ujumbe wa kuwasuta wasanii wa gospel wenzake. Ben C kupitia kibao hiki ambacho ndio gumzo nchini Kenya kwasasa kwa jinsi alivyowachamba wasanii kama Bahati Kenya, Willy Paul nawengine wengi, anasema kuwa wasanii wa muiziki nchini Kenya wamegeuza katiba ama maudhui ya hao kuitwa wanamuziki wa nyimbo za injili. Kwani wengi wamekua wakihaha na kutoka nje ya maadili ya kanisa nakuingilia mambo ya kidunia kwa kufanya nyimbo na wasanii ambao siwalokole, huku wakijitetea kwa maneno yasio kuwa na msingi wowote.

Ben C si mgeni kwenye tasnia ya muziki wa injili, na hata ameshawahi kuchaguliwa kuwania tuzo maarufu za gospel Africa Mashariki za Groove Awards 2017, katika kipengele cha Msanii mpya bora wa mwaka 2017. Japo tunzo hiyo iliikosa, msanii huyu amekuwa na bidii ya mchwa na kazi zake za muziki zimesheheni katika mtandao wake wa Youtube. Hizi ni baadhi ya nyimbo zake Nyasae, Similar, Hatudai na zinginezo nyingi tu ambazo zinapatikana katika chaneli yake ya Youtube tafadhali ipitie ili kufurahia kazi zake zaidi. Chini hapa ni baadhi ya picha zake, hebu burudika kwa kuzitazama.

 

Comments

comments

You may also like ...