Header

MAPRODUCER  WA KENYA EMMY DEE NA MWENZAKE AMZ WAUNGANA KUFANYA KAZI PAMOJA!

Palipo na niya siku zote hapakosi kuwa pana njia, na pia walilonga walumbi kuwa palipo na wazee hapakoseki jambo. Nayamugambo ikilia basi pana jambo. Nakupeleka hadi nchini Kenya kule mjini Mombasa, Mombasa mji wa kale kunani Mombasani? Muziki wa nchini Kenya haswa ule unaotengenzwa mjini Mombasa huwa hauna tofauti kubwa sana na wahapa nchini Tanzania, ndiposa huwa wakaazi wa jiji la Nairobi huwa wanaghaflika sana nakushindwa kutofautisha kati ya wasanii wa Bongo flava na wasanii wanaotoka ukanda wa Pwani ya kwao, yani wale wanamuziki wanao tokea miji kama ya Malindi, Lamu, Mombasa, Kwale na Taita Tavate yote haya ikichangiwa na utumizi wa lugha sanifu ya Kiswahili kwenye mashairi ya muziki tofauti na wasanii wanaotoka nyanda za juu za nchi ya Kenya nikimaanisha jiji la Nairobi na miji mingine kama vile Kisumu, Nakuru, Eldoret na mingine mingi inayopatikana sehemu hizi ambapo lugha ghafi ya Kiswahili borongi maarufu kama Shengi huwa inatumika.

Watayarishi wamuziki Emmy Dee (kushoto) na mwenzake Amz wakiwa kwenye pilka zao za kazi.

Sitaki nikuchanganye sana kwa kuleta mada nyingine katika makala haya, ila ninaona ni bora kujizatiti na kukudokolea ama kudurusu kuchambua mambo kwa kina kwa faida yako wewe shabiki wa habari zetu za burudani hapa DizzimOnline. Mtayarishi wa muziki na legendari katika tasinia ya muziki almaarufu kama Emmy Dee a.k.a Mshale bora mwituni, nikati ya watu wanaoheshimika kwasana nchini Kenya ikifika na maswala ya kutengeneza muziki. Mkono wake umewatoa wasanii tajika ikiwemo Sudi Boy na Dogo Rich miongoni ya wengine wengi tu. Wasanii wengi humuita mzazi mlezi wa vipaji, na anatajiriba kuu sana kiasi cha heshima yake sijui niielezeje. Ila kwa takribani miaka michache ya hivi karibuni, Emmy Dee alipotea kidogo kenye ramni ya muziki na kuwaacha wengi wakijiuliza mkongwe huyu kapotelea wapi?

Producer Emmy Dee

Sasa swali hili ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza kwa sana, kwasasa limepata jibu kwani Emmy Dee amerudi tena na sasa inaonekana ameshajipanga vizuri zaidi. Katika post zake za hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa facebook, Emmy anaonekana kana kwamba emeungana na mkongwe mwenzake na mtayarishi wa muziki producer Amz. Amz producer naye nikati ya malejendari wa muziki wanaofanya vizuri nchini Kenya na mkono wake ulishawatoa wasanii wakubwa wa nchini Kenya akiwemo msanii anayependwa na wengi hapa Tanzania Chikuzee. Kwahivyo ushirikiano  wa wakurugenzi hawa wazito wakutayarisha muziki wa kizazi kipya umefufua matumaini kwa wasanii na mashabiki lukuki nchini Kenya huku wengi wakingojea kwa hamu kujua nini hatua watakazo zichukua kupeleka muziki wa Kenya mbele mastaa hawa wawili.

Amz producer

Comments

comments

You may also like ...