Header

Major Lazer waja na ‘Tied Up’ wakimshirikisha Mr Eazi & Raye

Major Lazer wameachia wimbo mwingine uitwao “Tied Up” wakimshirikisha staa wa Nigeria, Mr. Eazi pamoja na Raye. Video ya wimbo huu ni ya tatu katika ushirikiano wa Major Lazer na muongozaji wa Afrika Kusini, Adriaan Louw.

“Tied Up” umekuja baada ya kutoka “Orkant/Balance Pon It” alioshirikishwa staa wa Afrika Kusini Babes Wodumo na “All My Life” alioshirikishwa Burna Boy. Pia ni wimbo wa tatu katika nyimbo za ushiriakiano kati ya Major Lazer na wasanii wa Afrika kipindi hiki.

Pamoja na hivyo, Major Lazer pia waliachia Afrobeats Mix mpya yenye nyimbo za wasanii wa Afrika ikiwa na lengo ya kuzipaisha kwenye majukwaa yao ya kimataifa.

Pia bendi hiyo inafanya ziara yake ya kwanza Afrika kwa kupita katika nchi za South Africa, Malawi, Kenya na Uganda.

Major Lazer pia watashiriki kwenye kampeni ya kutokomeza ujangili barani kwa kushirikiana na taasisi ya Veterans Empowered to Protect African Wildlife, VETPAW.

Comments

comments

You may also like ...