Header

Sallam SK kuipeleka Birthday Party ya Diamond Platnumz kwenye Mjengo Mpya

Meneja wa msanii wa muziki, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz, Sallam SK ‘Mendez’ ametangaza kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa msanii wake huyo kwenye nyumba yake mpya.

Ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Diamond Platnumz ambaye anatimiza umri wa miaka 29, Meneja Mendez kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe wa kumtakia maisha marefu na kuuchagua mjengo wake mpya kuwa ni sehemu atakayoitumia kusherehekea siku hii kabla ya ratiba nyingine kufuata.

“Happy Birthday mwanangu Chibu Dii Chibu Dee aka Mzee wa Multiple Choice aka Mzee wa maamuzi dakika za majeruhi!! Mie ni nani mpaka leo nisiandae Party ya kusherehekea siku yako ya kuzaliwa kwenye mjengo mpya!! Let’s everyone wish this kid @diamondplatnumz HAPPY BIRTHDAY and #morelife Ratiba zingine za kusherehekea siku yako ya kuzaliwa zipo pale pale #Tandale mjiandae na Jumapili pia Yatch Party tiketi zipo chache tu Dollar 500 tu msosi na vinywaji bureee!!! #PlatnumzBirthdayWeek.”.

Hata hivyo Diamond Platnumz ni kati ya mastaa wa wachache Tanzania wenye kuitumia siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwao kwa sherehe kubwa ambazo sambamba na Mipango kadhaa ya kibiashara uambatana na siiku hiyo.

Comments

comments

You may also like ...