Header

Arsenal kumkosa Mkhitaryan EUROPA, Chelsea, AC Millan uso kwa uso na Olympiacos

Burudani ya Michuano ya UEFA ndogo maarufu kama EUROPA league itarejea tena usiku kesho October 4 siku ya Alhamisi kama ilivyo kawaida ya ligi hiyo huku kivutio kikubwa kwa msimu huu kikiwa ni timu kubwa kutoka ligi ya Uingereza (PL) Chelsea na Arsenal ambazo zina mashabiki na wapenzi lukuki katika bara la Afrika na hasa nchini Tanzania zikiwa zinashiriki Michuano hiyo baada ya kushindwa kufuzu ile Mikubwa.

Arsenal itakuwa ugenini dhidi ya Qarabag FK katika dimba la Baku Olympic Stadium, Arsenal wataingia uwanjani bila kiungo wao Muarmenia Henrikh Mkhitaryan ambaye hataweza kuingia nchin Azerbaijan kutokana na uhasama baina ya nchi hizo mbili, huenda likawa Pigo kwao kutokana na uwezo wake aliionesha katika Michuano hii. ikumbukwe kuwa timu hiyo imeshinda mechi zao tano zilizopita katika mashindano yote na wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

Chelsea wao watakuwa nyumbani katika dimba la Stamford Bridge maarufu kama darajani wakiwakaribisha MOL Videoton ya Hungary. Chelsea wamepata matokeo ya kuridhisha tangu kuanza kwa msimu mpya chini ya kocha wao Maurizio Sarri. Eden Hazard anatarajiwa kuendeleza wimbi lake la upachikaji mabao kwa msimu kwani amekuwa na kiwango bora kabisa akiamua matokeo ya mechi kadhaa na za muhimu kwa timu yake kwenye Ligi kuu na Michezo mingine.

Mechi kubwa wiki hii huenda ikawa ni ile ya AC Milan dhidi ya Olympiacos katika dimba la Giuseppe Meazza, AC Milan bado hawajawa na makali yao ya zamani lakini wanaonesha kiwango kizuri katika ligi ya Italia, pia watakuwa bila mshambuliaji wao Gonzalo Higuain ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Michezo mingine ni RB Leipzig dhidi ya Celtic FC, Bayer Leverkusen dhidi ya AEK Larnaca FC, Fenerbahce dhidi ya FC Spartak Trnava, Anderlecht dhidi ya GNK Dinamo Zagreb,

Mbali na mechi za EUROPA burudani ya aina yake itakuwa Wikiendi hii katika jiji la Paris ambapo vinara wa Ligue 1, Paris Saint German watakuwa nyumbani dhidi ya mahasimu wao Olympic Lyon. PSG wana kikosi bora chenye wachezaji wenye majina na uwezo mkubwa lakini Lyon kikosi chao kinaundwa na Vijana wenye vipaji na uwezo vile vile, itakumbukwa msimu uliopita Lyon waliilaza PSG mabao 3-2 katika dimba hilo hilo. Macho yetu yataelekea Paris wikiendi hii huku mchezo ukiwa mubashara kupitia StarTimes ambao watarusha mechi zote za ligi hiyo.

Kumbuka Michuano hiI pendwa Duniani inarushwa Mubashara kupitita King’amuzi cha StarTimes pekee ambacho kina haki zote za Matangazo haya na Michezo hii unaweza kuipata moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi hicho.

Comments

comments

You may also like ...