Header

DOGO RICHIE ACHIA KIBAO KIMPYA KWA JINA MILELE

Msanii wa kutoka nchini Kenya almaarufu kama Dogo Richie a.k.a Rich Ree, amerudi tena kwenye ulingo wa muziki na kibao kipya na kikali kwa jina Milele. Akiongea na radio Citizen ya Kenya kwenye kipindi chenye ushawishi mkubwa Africa mashariki  Mambo Mseto kinachoendeeshwa na mtangazaji maarufu Africa Mashariki na Africa kwa ujumla Mzazi Willy M Tuva, Richie amefunguka nakusema kuwa mda huu ameamua kila atakapoachilia kibao kipya kitakuwa kinatoka na video yake kwa mpigo.

Dogo Richie akiwa na mtangaziji wa kipindi cha Mambo Mseto Mzazi Willy M Mtuva.

Dogo Richie ni miongoni ya wasanii wa nchini Kenya ambao wameweza kujizuia na kusimama imara kwenye ulingo wa muziki wa kizazi kipya japo kuwa kunachangamoto sihaba zinazowakumba wasanii wengi, kitu ambacho kimewafanya wanamuziki wengi wakubwa kuporomoka. Hata hivyo Dogo Richie tokea jana kupitia akaunti yake ya kijamii ya facebook, ameonekana akirusha picha za yeye akiwa pamoja na Msanii kutoka hapa Bongo Aslay. Kitu hiki kimezua gumzo mitandaoni nchini Kenya kwani wengi wanaohoji kuwa baada ya Aslay kuachilia kibao cha pamoja na Msanii Otile Brown kutoka Kenya pia basi huenda yuko mbioni kuingia studio na Dogo Richy. Aslay ambaye kwasasa yupo nchini Kenya kwa niaba ya kufanya burudani ndani mwa mji wa Eldoret Jumamosi hii, ameonekana mwenye bashasha na furaha kwani wakenya wengi wameondokea kumuelewa sana na kupenda si muziki wake pekee bali hadi hali jinsi maisha yake yanavyopanuka kila uchao. Show hiyo pia inasimamiwa na kudhaminiwa na Mseto East Africa ambayo inawwakilisha na Mzazi Willy M Tuva.

Aslay na Richie Ree wakiwa katika ubora wao.

Comments

comments

You may also like ...