Header

EMB Records yamsaini msanii wa kike ‘Princess Leo’, Aachia wimbo wa kwanza ‘Jionyeshe’ na Bahati

Lebo ya muziki ya ‘EMB Records’ inayomilikiwa na Msanii wa muziki Bahati kutoka nchini Kenya, imemsaini msanii mpya wa kike ‘Princess Leo’ na kuachia wimbo wake wa kwanza chini ya lebo hiyo, unaokwenda kwa jina ‘Jionyeshe’.

Princess Leo anakuwa msanii wa pili wa kike kusainiwa na lebo hiyo baada ya Rebecca Soki aliyeingika kwenye mkataba mwanzoni mwa mwaka huu. Wimbo mpya uliotoka wa Princess Leo umemshirikisha Bahati kwa utayarishaji wa Producer Paulo na video yake kuongozwa na Director Rahim.

Rebecca Soki

Tazama video ya wimbo huo hapa chini.

Kwa sasa lebo hiyo inaendelea kufanya kazi na wasanii kama Mr Seed, David Wonder na Rebecca Soki.

 

 

Comments

comments

You may also like ...