Header

Khaligraph Jones aingia Location kufanya Video Nchini Marekani

Rapa kutoka nchini Kenya, Brian Robert Ouko a.k.a Khaligraph Jones ameonekana akishoot Video ya wimbo wake mjini Dallas, Texas nchini Marekani.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Papa Jones aliweka Picha aliyoonekana akiwa Location na Mrembo(Video Queen), ‘Persian Barbie’ na kuzungukwa na baadhi ya watu walihisiwa kuwa sehemu ya utengenezaji wa video ya wmbo wake.

Khaligraph Jones aliweka picha nyingine kwenye ukurasa wake wa Instagram ilidhaniwa kuwa ni moja ya picha kutoka kwenye video anayotengeneza nchini Marekani. Khaligraph anatarajiwa kuhudhuria utoaji wa tuzo za Afrimma 2018 zitakazofanyika wikiendi hii, katika ukumbi wa House of Blues Dallas, Texas.

 

Comments

comments

You may also like ...