Header

Picha ya Diamond Platnumz na Kim Nana yamtoa Maneno Maimartha wa Jessy

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz baada ya kurudisha mkono wa shukrani kwa wanaTandale ‘Thank You Tabdale’ wiki iliyopita katika kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, Sherehe ziliendelea mpaka wikiendi iliyopita ambapo sherehe ilipewa jina la ‘Platnumz’s All white Party’.

Sherehe hiyo iliyofanyika kwenye Yatch kwenye ufukwe wa Bahari ya Indi, iliwakutanisha baadhi ya wasanii kutoka Lebo yake ya Wasafi ambao ni pamoja na Mbosso, Lava Lava, Rayvanny, Queen Darleen pamoja na Ndugu, jamaa na wafanyakazi wake wa karibu.

Katika Party hiyo, Diamond Platnumz alizungumziwa zaidi kutokana na kipande cha video alichoonekana akicheza kwa ukaribu na Mwanadada Mwanamitindo na Video Vixen kutoka Tanzania, Kim Nana hata wengine wadai kuwa inawezekana kuwa wawili hao wako katika mahusiano ya kimapenzi.

Kati ya waliojitokeza kuhusisha ukaribu wao na mahusiano ya kimapenzi ni Mtangazaji na majasiriamali, Maimartha Jessy ambaye aliweka Picha ya Mrembo Kim kwenye mukurasa wake wa Instagram na kuandika hivi :-

“Hapo vipi….🔥🔥
Tumepatia au tumekosea …
Naomba mumtag Wifi mupyiyaaa…….wifi wa Taifa….
#chombo kipya cha Nassib🤔
Dondosha comment yako…
@diamondplatnumz
Ataisoma….
Ukiwa na kaka usiogope wifii🤔
#nolocalpeople”.

Hata hivyo Mwanamitindo Kim Nana na Diamond Platnumz walishaonekana tena kwenye picha zilizowaonesha kuwa karibu katika Party za muoendelezo wa Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa wa Staa huyo aliyetimiza umri wa miaka 29 tarehe 2 Octoba mwaka huu.

Unadhani hili linaweza kuwa na ukweli au Kuna kilichojificha nyuma ya Kim Nana na Simba ‘Diamond Platnumz’.

Post ya Maimatha.

Comments

comments

You may also like ...