Header

Uhondo mwingine wa UEROPA, Arsenal, Genk ya Mbwana Samatta ndani.

Mashindano ya EUROPA Mzunguko wa Tatu yanaendelea tena hii Leo , UEFA Europa League inafahamika kwa kuwa na ushindani wa hali ya juu lakini kuwa na matokeo yasiyotabirika kiurahisi.  Moja kati ya Michezo inayotazamwa kuwa Mgumu sana ni Mchezo wa Sporting CP na Arsenal unatarajiwa mkali sana hasa ukizingatia kiwango cha Arsenal kwa sasa, lakini pia kiwango kizuri cha miamba kutoka Ureno ambao wana faida ya kuchezea uwanja wao wa nyumbani wa Jose Alvalade.
Michezo mingine itakayopigwa usiku wa leo ni RB Leipzig vs Celtic FC, Anderlecht vs Fenerbahce, AC Milan vs Real Betis, Olympic Marseille vs Lazio, pia Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya FC BATE Borisov.
Kivutio kingine ni timu anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta, Genk ambayo itacheza ugenini dhidi ya Besiktas ya Uturuki. Mbwana Samatta amekuwa na kiwango kizuri sana akiichezea klabu yake lakini pia timu ya taifa ya Taifa Stars, wengi watapenda kumuona akiendeleza kiwango chake katika Usiku wa Europa dhidi ya Besiktas.
Mbali na ligi ya Europa, wikiendi hii ligi ya Ujerumani itaendelea kwa mechi mbalimbali ikiwemo ile ya RB Leipzig na Schalke 04 itakayochezwa saa 11:30 jioni siku ya Jumapili katika dimba la Red Bull Arena na Utarushwa.
Huko Ufaransa katika Ligue 1 kutakuwa na mchezo mwingine wa kukata na shoka ambapo mabingwa Paris Saint Germain watakuwa wageni wa Olympique Marseille katika uwanja wa Orange Velodrome. Mara ya mwisho walikutana mwezi wa pili ambapo Marseille walifungwa mabao 3-0. Marseille watamkosa mshambuliaji wao Florian Thauvan ambaye anauguza majeraha. Mchezo huo pia utaonyeshwa moja kwa moja kupitia World Football saa 5 Usiku siku ya Jumapili.
Kumbuka Michezo hii itakua Live kupitia Kingamuzi chako cha DStv ambacho kitakuletea burudani hizi mubashara tena kwa kiwango cha HD na baadhi ya Michezo itatangazwa kwa Lugha ya kiswahili mfano ile ya Bundesliga.

Comments

comments

You may also like ...