Header

MAKALA: WEMA SEPETU ANAHITAJI USAIDIZI LAKINI SI KUSUTWA!

Kama ilivyo kwa kila binadamu, huwa anamapungufu ya kwake. Mwenyezi Mungu katuumba sote ila hatayeye anajua sisi siwakamilifu. Katika makala yangu ya leo, nataka kunakili matukio yote ambayo yameweza kutokea kwa mkurupuko nakuweza kutengeneza vichwa tofauti vya habari si nchini Tanzania pekee, ila hadi Kenya na eneo zima la Africa Mashariki na maziwa makuu. Moja kati ya habari hizi ni kuhusu mrembo wa Tanzania ambaye kwa uwezo wa wengi na upendo wa mashabiki wake wengi nchini ameweza kupewa taji la kuwa ”Tanzania Sweetheart” ama kwa lugha ya Kiswahili ”Kipenzi cha Watanzania.

Kupitia video aliyoachilia hadharani iliyomuonyesha nyota huyu wa filamu akilishana denda na kwa yule anayedai kuwa ndiye mpenzi wake mpya kwa jina Patrick, Wema amezua hoja kubwa ambayo imempelekea yeye kuweza kuita mkutano na vyombo vya habari nakuomba radhi kwa jamii kwa kitendo kile alichokifanya. Japo hatayeye mwenye amekiri kuwa kakosea, anajua fika kama ilivyo ada ya waja, wengi wataitumia fursa hii na makosa yake mwenyewe kumukaanga kwa kikaangio cha mafuta ya moto. Lakini kwa upande wangu kama muandishi, ninakila sababu za kuwaomba wengi waweze kumuelewa Wema Sepetu kwani hali anayopitia sio ya kawaida na kwa umaarifu alionao huenda ikawa sababu moja wapo ya mchango wa masaibu anayoyapitia mwanadada huyu. Niko na vipengele kadhaa amabvyo vitakuwa vinasimamia sababu kuu yangu yakutaka watu wamusaidie Wema ila sikumsuta.

  1. MAPENZI YA DHATI, KISASI NA KUVUNJWA MOYO

Wema Sepetu anatokea kuwa mwanadada mwenye mapenzi ya dhati. Hii inatokana na mahusiano yake na msururu wa wapenzi wake wote wa awali aliotokanao kimapenzi. Hata siku moja haijawahi tokea kuwa Wema alishawadaganya wala kutoka kimapenzi na mwanaume mwingine wa kando wakati yeye yupo kwenye mahusiano. Bali hutokea wapenzi wake ndio huwa wanachepuka na wanadada wengine akijagundua Wema ndipo huwatema na kuwachana na wanaume hao kwa uchungu. Na kwakutokana na kuvunjwa moyo na wanaume ama wapenzi hawa, Wema huwa mrahisi wakutaka kulipisha kisasi. Sasa hapa ndipo shida hutokea, kwani mrembo huyu huchanganyikiwa kabisa.

Wema akila raha na mpenzi wake mpya

Basi iwapo wakati huu ambao huwa nahaha kulipa kisasi kwa kudanganywa na kuvunjika moyo na mtu ambaye ana mwamini na mara atokelezee mwanaume yeyote yule amufurahishe tu japo hata ikawa kwa mda wa mwezi mmoja, Wema huitumia fursa hiyo ili kumuadhibu aliyemvunja moyo. Dhamira kuu ya kufanya hivi naona huwa anataka kuonyesha kuwa yeye pia ananguvu ya kufanya maamuzi kama wanaume wanavyofanya. Ila husahau kuwa hii ni Africa, itikadi na tamaduni zetu hazimruhusu mwanamke kuchepuka na zaidi ya wanaume zaidi ya mmoja kama vile wanaume wanavyofanya.

Na matokeo yake huwa kama ilivyo kwasasa, nikilipigia msasa wazo hili nikuwa, Wema kwa mara ya mwisho alikua anatoka kimapenzi na mshindi wa BBA Idris Sultan. Hatuwezi jua nini kilichotokea, ila sio siri tena tukisema walishaachana. Japo Wema alishaonyesha kutulia kwa mda, na hata akaonekana kuwa na ukaribu na mpenzi wake wa zamani na rafiki yake wa karibu ambaye ni Diamond.

Wema akiwa pamoja na Idris Sultan

Ndani yake inaonekana alikua anaugua kwasana. Ukumbuke Idris alishawahi kutupia picha na pia video akila raha na mrembo mwenye asili ya kizungu huku wengi wakitafsiri kuwa huenda akawa ndiye mchumba wake mpya aliyeziba nafasi yake na dadake Wema. Hivyo Wema kwa upande wake alihitaji kujibu pigo hili, ila kwa upande wake imemchukua mda mrefu kumpata mtu huyo. Ila alipokuja wakuitwa Patrick basi siha na tabia zake ambazo wengi tunazifahamu zakutoficha yake ya sirini Sepetu akasepetuka na video ya mahaba niue. Chambilicho picha za awali zilizozua utana na pia zilizotumika kama silaha ya kumuadhibu Diamond wakati walipokosana na Wema na zilizosababisha Diamomd na Ommy Dimpolez kukosana wakati Ommy na Wema walipokua katika harakati za kutengeneza video ya Wanjera ambapo Wema alitumika kama  video vixen.

 

2. KUHAHA KUPATA MTOTO

Wema Sepetu si mara moja amekua akililia kupata mtoto. Katika mahojiano yake na vyombo tofauti tofauti vya habari, mrembo huyu amekuwa akilijadili swala hili kwa kina. Kwa mara ya mwisho akilisimulia hili, ilikua kwenye show ya The Play List pale Times FM na Dj Lily Ommy. Nikimunukuu maneno yake, ” Swala la mimi kupate mtoto, ni swala gumu sana. I have been wishing to get my own child tangia nikiwa na umri wa miaka 21. I was thinking like, kama ningekua nimepata mtoto wakati ule sasa ningekua ama having something to show off, lakini now am turning 30 but sijafanikiwa ila am still having hope kwakuwa tatizo langu lilipata daktari kutoka India na soon nitaweza kuitwa mama. Am longing for that moment.” alilalama Wema.

Dj Lil Ommy akiwa na Wema Sepetu

Wema aliangazia kuwa kunakipindi alikuwa yuko radhi kunywa dawa yoyote ilimradi tu kama ingemwezesha yeye kupata ujauzito. Sasa kwa kauli yake hii, inaonyesha Wema kwa hivi sasa yeye haangalii monekano wa mwanaume tu kwa nje, ama kufata utajiri wa pesa, kwani pesa ninini kwake? Ila yeye anachoangalia ni lile swala la ninani yule mwanume atakayemwezesha kuumpa ujauzito angalau nayeye aondokelewe na aibu yakuwaitwa tasa. Mahadui wake wengi, wamekuwa wakiitumia kutozaa kwake kama ncha ama silaha madhubuti ya kumpigia, kitu ambacho kimemufanya Wema Sepetu kuumia nakulegeza nyege kwa kila mwanaume atakaye mdanganya na kumuahidi kumpa ujauzito pindi tu yeye atakapokubali kutoka naye kimapenzi.

Wema anaumia, pia anasumbuka sana. Si kwaupande wa sanaa pekee ila pia kisaikolojia, anahitaji upendo wa dhati na marafiki watakao mpenda nakumuelekeza kuliko kwema kama ilivyo na jina lake. Kama watanzania mlivyompa taji la kuwa ”The Tanzanian SweetHeart basi kazi kubwa itakua kumuonyesha upendo wa dhati na kumsamehe kwa kile chochote anachokosea haswa upande wahisia zake kwa upande wa mapenzi. Japo ya umaarufu wake, yeye pia ni binadamu kama wewe na mimi, anaweza kuumia, anaweza kulia, anaweza kuchanganyikiwa kimaisha kama wewe na mimi na pia kutapeliwa na matapeli wa mapenzi ambao wapo wengi tu hapa mjini. Kwahivyo kama alivyoomba radhi kwa jamii, basi jamii inafaa kumsamehe na kumuombea Mungu amtimizie hoja ya moyo wake ambayo ameeitamani kwa miaka na mikaka. Kutoka kwangu hapa nchini Kenya, ni mimi mwandiishi wako na mchnganuzi wa mambo ya burudani….niite Changez Ndzai.

 

Comments

comments

You may also like ...