Header

Vita ya Wababe Wikiendi hii Bundesliga, Ligue 1

Wikiendi hii ni mzunguko mwingine wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga na miongoni mwa michezo ambayo itakuwa ya kuvutia sana ni ule wa RB Leipzig dhidi ya Hertha Berlin. Leipzig hawajashuka sana ukilinganisha na kiwango walichokuwa nacho msimu uliopita, Hertha Berlin pia wana msimu mzuri hadi sasa ikiwa ni tofauti tu ya magoli ndiyo inawatofautisha na Leipzig ambao wako nafasi ya tano kaatika msimamo wa ligi, Hertha Berlin kwa sasa wanatamba na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Salomon Kalou ambaye amezidi kudhihirish kuwa umri ni namba tu, wiki iliyopita alifunga mabao mawili katika droo dhidi ya vinara wa ligi hiyo Borussia Dortmund. Kalou anatarajiwa kuwa tishio tena katika mchezo huo wa wikendi hii.
Michezo mingine katika ligi ya Bundesliga wikiendi hii ni Bayern Munich vs Freiburg, Schalke vs Hannover, Bayern Leverkusen vs Hoffenheim, Wolfsburg vs Borussia Dortmund na siku ya Jumapili ni Borussia Monchengladbach vs Dusseldorf na Mainz vs Werder Bremen.
Napo katika ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 wikendi hii michezo kadha wa kadha itapigwa katika viwanja vikubwa kwenye ligi hiyo, mabingwa Paris St Germain wanacheza usiku wa leo dhidi ya LOSC Lille saa 4:45 Usiku Mubashara kupitia ST World Football, PSG wanacheza katika kiwango bora kabisa kwa sasa huku wakijivunia nguvu kazi ya washambuliaji wao kama mbrazil Neymar, kinda wa Ufaransa Kylian Mbappe na fowadi wa Uruguay Edinson Cavani ambao ni tishio kwa safu yoyote ya mabeki kwa sasa.

Kumbuka Michezo yote hii itakua Live kupitia king’amuzi cha StarTimes ambacho kina dhamana ya kurusha Michezo hii  tena kwa lugha ya Kiswahili

Comments

comments

You may also like ...