Header

Majibu ya Uvumi wa Mitandaoni kuhusu TECNO kuwabadilishia Wateja wao SIMU ya CAMON KWA CAMON 11 MPYA

ikiwa zimebaki siku chache kufunga mwaka 2018 kuna tetesi mtaani kuwa kampuni ya simu za Mkononi ya TECNO imewaandalia watumiaji wa simu za TECNO camon ofa,  na hii inakuja kutokana na uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba kila mtumiaji wa TECNO camon atapata ofa ya kubadilishiwa simu yake ya camon kwa camon 11 mpya.

Mbali ya kwamba TECNO inamatoleo ya simu yenye hadi megapixel 24 (Camon x pro) bado inasemekana kutoifikia au hata kuikaribia kamera ya camon 11 inayodhaniwa kuja na teknolojia ya Artificial intelligence. Na endapo hizi tetesi za camon 11 kuwa na teknolojia ya Artificial intelligence zikawa na ukweli wowote basi camon 11 ni zaidi ya camon zote katika upande wa kamera. Lakini pia huenda camon 11 ikaja na kioo cha nchi 6.2HD+ au zaidi chenye teknolojia ya notch.

Tetesi ya camon 11 kuja na ofa ya kubadilisha simu inasemekana imelenga zaidi watumiaji wa TECNO camon cx, camon cm, camon x na camon xpro.

Comments

comments

You may also like ...