Header

Harmonize, Jux, Mimi Mars, Nandy na wakali wengine kutoka Afrika kuupamba kwa Burudani Msimu Mpya wa Coke Studio 2019

Majina ya zaidi ya 25 ya wasanii wenye vipaji toka barani Afrika yametajwa kutokea kwenye msimu mpya ujao wa ‘Coke Studio Africa 2019 utakaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya. Wasanii na watayarishaji wa muziki kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Nigeria na nchi zingine kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika watahusika kuandaa muziki lengo likiwa ni kuwaburudisha wapenzi muziki.

 

Burudani hiyo itashuhudiwa kupitia kipindi kitakachoanzakuruka kwenye kioo cha televisheni yako kote barani Afrika kuanzia mwezi Februari 2019. Kwa mara nyingine tena, wapenzi wa kipindi watapata kushuhudia msisimko wa  mchanganyiko wa muziki, marudio ya nyimbo za zamani, na utengenezwaji wa nyimbo mpya.

Kama “Vimbada” toka kwa Mkali wa nchini Kenya Moji Short Baba atashiriki Coke Studio Africa kwa mara ya kwanza akiwa na Naiboi, kwa sasa anatamba na kibao chake cha “2 In 1”, Mkali wa Michano ya (Hip-Hop) Khaligraph Jones, ambaye hivi karibuni ametwaa tuzo ya kuwa mwana muziki bora wa Hip-hop barani Afrika mwaka 2018 katika tuzo za AFRIMMA, atarudi kwa mara ya pili katika msimu huu mpya. Kutoka Tanzania msanii nyota wa bongo flava na mshindi wa tuzo ya BET Rayvanny  pamoja na mwanadada hitmaker wa wimbo ‘AIBU’, ‘Nandy’ atashiriki kwa mara ya pili.

 

Baadhi ya washiriki wapya ni Mkali wa wimbo ‘Kwangwaru’, Harmonize na Juma Jux, mkali wa muziki wa R&B na msanii kutoka Mdee Music, Mimi Mars. Uganda watawakilishwa na Sheebah ikiwa ni mara yake ya pili kushiriki. Ataungana na wasanii maarufu mbali mbali wa nchini Uganda akiwemo Mahelt, na wenyeji kama Bisrat, Abush Zekele, Yared Negu na Rophnan Nuri.

Khaligraph Jones

Ladha ya burudani toka Magharibi mwa Afrika italetwa na watayarishaji wakali wa muziki, GospelOnDeBeat na nyota wa muziki nchini Nigeria Skales na Rude Boy watakao ling`arisha jukwaa kwa utumbuizaji wa hali ya juu na vibao matata.

Rude Boy

Utayarishaji wa Coke Studio Africa 2019 unaendelea, kwa nyimbo za kushirikiana za wasanii na waandaaji wa muziki watakao tengeneza muziki utakao waunganisha watu kutoka barani  Afrika. Itahusisha zaidi ya nyimbo halisi 10 zilizotengenezwa na mtiririko wa kipekee kwa msimu Chrisimass kwa mwezi huu wa Disemba 2018 kutoka coke studio Afrika.

 

Comments

comments

You may also like ...