Header

IFAHAMU KWA KINA TAMTHILIA MPYA YA PETE KUTOKA KENYA!

Pete ni tamthilia inayoangazia maisha ya ndugu au kaka wawili (Mbura na Jasiri) ambao baada ya kifo cha kiongozi wa kisiwa cha Funzi ambaye ni baba yao (Mz Dalu), walianza kung’ang’ania uaongozi. Uongozi huo uliibua chuki, ubinafsi, vitimbi na visasi kati ya ndugu hao wawili. kisiwa kikagawanyika pande mbili…Je, ni nani atafaulu kuuchukua uongozi? hilo ndilo swali tamthilia ya pete inajaribu kulitafutia jibu. Wakati sanaa ya uigizaji inavyozidi kukua Africa, Africa Mashariki imekua miongoni mwa nyanda zinazojenga Africa zilizokatika mstari wa mbele kuhakikisha sanaa inaliweka bara hili katika ramani ya dunia. Muziki umethhibitisha hili tayari, ila kiwanda cha filamu kwasasa pia kinajizatiti kuhakikisha kinapeana nafasi za juu na kutebgeneza upenyo wa kazi kwa vijana lukuki Africa.

Mdau wa filamu kwenye filamu ya pete Yusuf Dalu na muigizaji mwenza mwanadada Stephanie Maseki ambaye ameiga kama Amina.

Akiongea na meza yetu ya habari, mmoja wa wahusika wakuu wenye kuitengeneza filamu ya PETE akiwa Mombasa Bwana Yusuf Dalu, ameiambia Dizzim kuwa, filamu ya PETE imekuja kuibadilisha taswira ya filamu si hapa Africa Mashariki pekee bali bara zima la Africa na anafurahia tayari kupitia channel ya televisheni ya MAISHA MAGIC EAST lengo lao kuu limeanza kutekelezwa. Mfumo muzima wa kutengeneza filamu nchini Kenya, umeleta mabadiliko makuu katika kiwanda cha sanaa, na tofauti na hapa nchini Tanzania ambapo muziki ndio unaongoza, Kenya kiwanda cha filamu ndicho kinacho ongoza. Je ungetamani kuwafahamu na kutengamana na mastaa wa filamu unaowapenda kutoka nchini Kenya? Basi usiwenashaka, kupitia Dizzim Online tutakuwa tunakuandalia taarifa kuhusu mastaa wa filamu kutoka Africa Mashariki na Africa kwa jumla ili kuleta mvuto na kuongeza  utamu zaidi kwenye burudani letu kupitia mtandao huu wakipekee Africa Mashariki. Tazama picha za uzinduzi wa filamu hii hapa chini kutoka mjini Mombasa kwenye viwanja vya Pirates Beach.

Wacheshi maarufu Erick Omondi na Chipkizy wakiwa ulingoni katika uzinduzi wa filamu ya Pete.

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...