Header

Juventus kuendeleza Ubabe Coppa Italia? Bologna watayafanya kama ya Guingamp kwa PSG?

Katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Coppa Italia ni timu mbili tu zinatoka Serie C huku zikikutana na vilabu kutoka jijini Roma, Novara watakaocheza dhidi ya Lazio huku Virtus Entella wakicheza dhidi ya AS Roma siku ya Jumatatu.

Timu nyingine ambayo haitokei Serie A ni Benevento ambao watasafiri kuelekea Milan ambako watacheza dhidi ya Klabu kongwe ya Inter Millan.

Huku ikitarajiwa kwamba vilabu vingi vikubwa vitashinda, mechi kati ya Bologna na Juventus itakuwa kivutio zaidi. Juventus tayari wako kileleni kwenye Serie A wakiwa mbele kwa  alama 9 zaidi ya Timu inayoshika nafasi ya Pili Klabu ya Napoli.

Klabu hiyo kutoka  jijini Turin itataka kujihakikishia ushindi dhidi ya Bologna ambao ni wa tatu kutoka mwisho katika msimamo wa Serie A, ili wawe katika nafasi nzuri ya kushinda kombe hilo kwa mara ya 14.

Kikosi cha Massimilano Allegri bado hakijapoteza mchezo wowote katika ligi za ndani kwa msimu huu, huku kikosi chao kikiwa na utajiri hasa eneo la ushambuliaji wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Paulo Dybala na Mario Mandzukic, itakuwa jambo la kushangaza endapo watapoteza mchezo huo licha ya kuwa ugenini.

Ronaldo amefunga jumla ya magoli 14 katika ligi, goli moja pungufu ya magoli ambayo kikosi kizima cha Bologna kimefunga (15), mreno huyo amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipowakacha mabingwa wa Ulaya Real Madrid.

Mchezo mwingine wenye burudani utapigwa jijini Genoa ambapo Sampdoria watacheza dhidi ya AC Milan siku ya Ijumaa.

Wapenzi wa Soka nchini wataweza kutazama mechi hizi kupitia StarTimes pekee. Mechi kati ya Bologna na Juventus  itachezwa Jumapili saa 2 Usiku na kurushwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee kwa watumiaji wa Antenna na Dish.

Comments

comments

You may also like ...