Header

Alicios Theluji ampa Shavu kubwa Jay Melody kutoka Tanzania

Msanii wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Alicios Theluji ‘Queen Alicios’ amempa shavu mwandishi wa muziki kutoka Tanzania, Jay Melody kwenye wimbo wake mpya unaotarajiwa kutoka wiki Ijayo.

 

Queen Alicios pamoja na uongozi wake walikubaliana kuachia wimbo mpya utakao kwenda kwa jina ‘Nitadata’ ikiwa ni kazi yake ya kwanza kwa mwaka 2019. Wimbo huo umetayarishwa na Producer ‘Ihaji Made It’ wa nchini Kenya.

Jay Melody

Jay Melody mbali na kujihusisha na uandishi wa nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri kwenye tasnia ya Burudani nchini Tanzania pia ni kati ya wasanii wanaotajwa kufanya vizuri kwa nyimbo ambazo tayari zimetoka ambazo ni pamoja na Goroka, Namwaga Mboga, Sana na nyingine nyingi.

 

Katika Post hapa Chini Inadaiwa kijana huyu mwenye kujengeka misuli ni kati ya watakaoonekana kwenye video ya wimbo huo.

Video ilifanyika nchini Tanzania chini ya Director Jowzey nchini Tanzania. Wimbo huu utakuwa ni wimbo wa pili kutoka kwa Queen Alicios akiwa nje ya usimamizi wa lebo yake ya zamani ya Taurus Musik ya nchini Kenya.

Comments

comments

You may also like ...