Header

DOGO RICHY AMUSIFIA MZAZI WILLY M. TUVA ASEMA SIMUNAFIKI!

SHARE:

Masanii Dogo Richy

Msanii  Dogo Richy ambae anatamba vyema na kibao chake kipya kwa jina Ngojea, amemulimbikizia mtangzaji wa redio na runinga wa kitua cha habari nchini Kenya cha Citizen maarufu kama Mzazi Willly M. Tuva sifa chungu nzima. Richy ambaye weeknd hii alikua mwenyeji wa msanii Aslay mjini Mombasa, amesema MC wasiku hiyo Mzazi Tuva kama wengi wanvyomutmbua ana upendo wadhati didhi ya wasanii wa muziki na wala hana fitina na majungu. Amewataka wadau kwenye sekta ya muziki Africa Mashariki wawe na miondoko kama ya Tuva ilikuusukuma muziki wa Africa Mashariki juu zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Dogo Richy ametumia mda wake kuandika maneno haya ”One thing ambayo Mzazi Willy M. Tuva napenda hafake upendo kwa MTU yoyote ile introduction alonifanyia Talentos ilikua lazima fan akuskize…jina LA mzazi kweli halikuja bure GOD bless u ..tusiwe watu wakufake uwe natabasam kwa uso kumbe moyoni umekaba…hata MUNGU ndio huyu msee amefika hapa alipo”. 

 

Mzazi Tuva Akiwa Na Vanessa Mdee Kwenye Studio za Radio Citizen Kenya

Tuva hatahivyo amekua msaada na daraja la kuwavusha wasanii wengi Africa Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Awali msanii Diamond ameshawihi kukiri kwamba kupitia kipindi cha Mambo Mseto kinacho endeshwa na Willy M. Tuva kila siku ya wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, kuwa kilihusika pakubwa katika kuifikia ndoto yake yakua staa mkubwa wa muziki barani Africa. Hata hivyo wasanii wengi wamekuwa wakimsifia mtangazaji huyu ambaye wengi wanamuona kama mlezi wa vipaji vya muziki Africa Mashariki. Chini tazama video Diamond akiongelea kuhusu vile Mzazi Tuva alivyo msaidia kupitia kipindi cha Mambo Mseto.

Comments

comments