Header

Diamond Platnumz kuzama mahakamani kwa kesi nzito na Hamisa Mobeto

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ameingia katika songombingo la mtoto wake wa tatu ‘Abdul Naseeb Juma’ aliyempata na mrembo Hamisa Mobeto baada ya kutapakaa taarifa za kuwa kuna ripoti ya kufunguliwa kwa mashtaka na kutoka kwa wito  juu ya malalamiko kuwa ameshindwa kutimiza jukumu lake la kutoa matunzo ya mtoto.

Kwa mujibu wa wakali Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, katika mzungumzo na chombo cha habari cha Mwananchi siku ya Alhamisi ya wiki hii Zulu amesema kuwa mteja wao ambaye ni mzazi wa mtoto wa tatu wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobeto alimtumia Diamond ilani ya awali ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba taarifa zilizoonesha kuwa inawezekana Diamond alikatisha huduma hiyo kiasi cha mashtaka hayo kupelekewa Mahakama ya Kisutu upande wa watoto.

 

Wito unaomkabili Diamond Platnumz unasimama katika madai ya kumdhalilisha na kutompa Hamisa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili sasa na kwa mujibu wa wakili Zulu tayari wakili wa msanii Diamond ameshapokea wito huo na ameongeza kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...